MULTICULTURALIM 2021
Tuesday, 21.03.2023, 05:55
» MAIN MENU
» STATISTICS

Total online: 1
Guests: 1
Users: 0


free counters

Hamjambo, wasemaji wa Kiswahili !

Nilizaliwa nchini Urusi nikafanya masomo yangu nchini Ufaransa. Tangu zamani nilikuwa na hamu ya kujua zaidi juu ya nchi za kiafrika na kusikiliza miziki ya kiafrika niliougundua mwanzoni mwa miaka 90s. Kabla ya mwaka wa 1996 Kiingereza kilikuwa lugha ya kigeni moja tu niliyoizungumza, ndiyo sababu nilianza kujifunza lugha nyingine za kigeni baada ya kujiunga na chuo kikuu. Nilichagua lugha ya Kiswahili kwa sababu ni lugha muhimu zaidi katika Afrika Mashariki ambayo ni sehemu ya bara la Afrika inayopendwa sana na watalii. Ujuzi wa lugha hiyo ulinisaidia sana kuwasiliana na kufanya marafiki na wanafunzi wengi kutoka Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda na hata sehemu za mashariki za Kongo kuanzia mwaka wa 1998. Wengi wao walikuwa ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Urafiki baina ya Mataifa nilikofanya kazi ya msaidizi wa msimamizi wa kitivo cha matayarisho kwa muda wa miaka miwili. Baada ya kupita mtihani wa Kiswahili mnamo mwezi wa desemba 2000 nilipata pendekezo kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje kuhusu nafasi ya kazi kwenye Russian Cultural Center mjini Dar Es Salaam (Tanzania), lakini nilifanya uamuzi kuendelea na masomo yangu ya uzamili nchini Ufaransa.

Kuanzia mwaka wa 2001 nilikuwa na mawasiliano machache sana na wasemaji wa Kiswahili kwa sababu wengi wao hawaendi Ufaransa, na pia kwa sababu nilikuwa sina nafasi tena ya kuwatafuta na kuwasiliana nao kwa njia ya mtandao. Hata hivyo, ninafurahi sana kuwa na uzoefu wa kuzungumza lugha hiyo maarufu na kutoisahau baada ya miaka hiyo yote ya ukosefu wa mawasiliano. Ninatumaini kupata nafasi tena ya kuitumia katika kazi yangu na mwishoni kuzuru bara la Afrika na kuwatembelea marafiki zangu ninaowafahamu tangu zamani.

» Activités extra-professionnelles
» MULTILINGUAL MENU

©2023 VLADISTRIBU